Ni lazima kupanda kwenye miamba wakati wa Sa´y?

Swali: Je, ni lazima kupanda kwenye miamba?

Jibu: Hili ni Sunnah, lakini kilicho wajibu ni kutembea kati ya Swafaa na Marwah. Hata hivyo kupanda ni Sunnah.

Swali: Je, apande kwenye mwamba wenyewe au sehemu ya juu iliyotandikwa marumaru?

Jibu: Jambo linalojulikana ni sehemu ambayo watu wanasimama sasa.

Swali: Ikiwa hakupanda kabisa?

Jibu: Ikiwa alizunguka kati ya Swafaa na Marwah, hiyo inatosha. Kupanda ni Sunnah tu.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24996/هل-يلزم-الصعود-على-الصخور-في-السعي
  • Imechapishwa: 24/01/2025