Swali: Masikini huyu ambaye watu hawamuoni endapo atasubiri wakati wa dharurah basi anadhurika na pengine akafariki.

Jibu: Hapana, anatakiwa kuomba.

Swali: Ni lazima kwake kufanya hivo?

Jibu: Ni lazima kwake kuikoa nafsi yake. Wakati haja inapelekea kufanya hivo kwa kuchelea kifo basi itamlazimu. Aidha ni lazima kwa ambaye anajua hali yake kumuokoa na kumpa.

Swali: Nakusudia endapo ataona kuwa inapendeza kwake kusubiri – itakuwa ni sahihi kufanya hivo au analazimika kuomba?

Jibu: Hapana kama yuko na kitu kidogo kinachoweza kukidhi mahitaji yake. Vinginevyo analazimika kuomba ili kuiokoa nafsi yake na walioko chini yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22267/حكم-المسالة-للمسكين-الذي-لا-يفطن-له
  • Imechapishwa: 21/01/2023