Du´aa ya safari inasomwa mtu anapokuwa katika mji wake au kwenye lifti?

Swali: Je, inapendeza kusema:

الله أكبر ، الله أكبر ، الله أكبر سبحان الذي سخر لنا هذا وما كنا له مقرنين ، وإنا إلى ربنا لمنقلبون ، اللهم إنا نسألك في سفرنا هذا البر والتقوى ومن العمل ما ترضى ، اللهم هون علينا سفرنا هذا ، واطو عنا بعده ، اللهم أنت الصاحب في السفر ، والخليفة في الأهل ، اللهم إني أعوذ بك من وعثاء السفر ، وكآبة المنظر ، وسوء المنقلب ، في المال والأهل

”Kwa jina la Allaah. Himdi zote njema ni stahiki ya Allaah. Ametakasika kutokamana na mapungufu ambaye ametuwepesishia haya na tusingeliweza wenyewe kuyadhibiti na hakika kwa Mola wetu tutarejea.” Ee Allaah! Hakika sisi tunakuomba katika safari yetu hii wema na kukucha na katika matendo unayoyaridhia. Ee Allaah! Ifanye nyepesi safari yetu hii na fupisha umbali wake. Ee Allaah! Hakika Wewe ndiye unayesuhubiana nami katika safari na mchungaji wa familia yangu. Ee Allaah! Hakika mimi najilinda Kwako kutokamana na ugumu wa safari, ubaya  wa mtizamo na mgeuko mbaya katika mali na familia.”

safarini na kwenye lifti?

Jibu: Wakati wa safari kama ya gari, meli na ndege.

Swali: Mtu anapokuwa katika hali ya ukazi?

Jibu: Hapana. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiisoma safarini. Alikuwa anapopanda chombo safarini ndipo anaisoma.

Swali: Vipi kwenye lifti?

Jibu: Safarini peke yake. Lifti sio safarini.

Swali: Kwenye chombo inasomwa wakati wowote?

Jibu: Wakati amesafiri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22266/هل-يقال-دعاء-الركوب-في-غير-السفر
  • Imechapishwa: 21/01/2023