Ameoga kwa ajili ya kujisafisha kisha akaswali ijumaa

Swali: Ikiwa mtu ameoga katika siku hii kwa ajili ya kujisafisha na sio kwa ajili ni siku ya ijumaa kisha akaswali swalah ya ijumaa. Ni yepi maoni ya sawa na twahara inaenea yote mawili?

Jibu: Hapana. Ikiwa hakutawadha haisihi. Ni lazima atawadhe wudhuu´ unaokubalika kwa mujibu wa Shari´ah. Lakini wanazuoni wengi wanaona akiwa na janaba na akanuia kuondosha yote mawili basi inaondosha hadathi zote mbili. Hapa ni pale ambapo anakuwa na janaba.

Swali: Kwa maana nyingine airudie swalah aliyoiswali kwa josho hili?

Jibu: Ndio, airudie kwa aina ya Dhuhr.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22265/حكم-من-اغتسل-للتطهر-فقط-يوم-الجمعة
  • Imechapishwa: 21/01/2023