Njia ya Salaf na Ahl-ul-Bid´ah wa zama hizi haisilihi?

Swali: Ni ipi hukumu ya ambaye anasema kuwa njia ya Salaf na Ahl-ul-Bid´ah na wahalifu wa leo haisilihi na anakimbiza mbali kutokana na simulizi zao?

Jibu: Kwa hivyo anachotaka ni nini? Anaposema kuwa njia ya Salaf haisilihi na wahalifu wa leo, ina maana kwamba wanataka kuleta Qur-aan na Sunnah vipya. Njia ya Salaf kwa wahalifu imejengwa juu ya Qur-aan na Sunnah ili kuwafanya wale wahalifu kuikubali haki. Hii ndio njia ya Salaf – imesalimika, wajuzi zaidi na yenye hekima zaidi.

Ama kuhusu njia ya wale waliokuja nyuma, sijui nini wanachotafuta kutoka katika njia inayovuka njia ya Qur-aan na Sunnah katika kuwaongoza watu. Yule asiyeongozwa na Qur-aan na Sunnah basi hatoongozwa na kitu kingine:

وَأَن لَّوِ اسْتَقَامُوا عَلَى الطَّرِيقَةِ لَأَسْقَيْنَاهُم مَّاءً غَدَقًا

”Kama wangelinyooka kwenye njia, bila shaka Tungeliwanywesha maji kwa wingi.”[1]

وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ

“Hii ndio njia Yangu iliyonyooka, hivyo basi ifuateni na wala msifuate njia zingine; zikakufarikisheni na njia Yake!”[2]

وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّـهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا

”Na shikamaneni kwa kamba ya Allaah nyote pamoja wala msifarikiane.”[3]

Kwa hivyo hakuna njia nyingine isipokuwa ya Salaf:

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ هَدَى اللَّـهُ ۖ فَبِهُدَاهُمُ اقْتَدِهْ

“Hao ndio ambao Allaah amewaongoa. Hivyo basi fuata kama kigezo mwongozo wao.”[4]

وَمَن يُشَاقِقِ الرَّسُولَ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُ الْهُدَىٰ وَيَتَّبِعْ غَيْرَ سَبِيلِ الْمُؤْمِنِينَ نُوَلِّهِ مَا تَوَلَّىٰ وَنُصْلِهِ جَهَنَّمَ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا

”Yule atakayempinga Mtume baada ya kuwa imeshambainikia uongofu na akaifuata njia isiyokuwa ya waumini, Tutamgeuza alikogeukia na tutamuingiza Motoni – na ni uovu ulioje mahali pa kuishia!”[5]

[1] 72:16

[2] 6:153

[3] 3:103

[4] 6:90

[5] 4:115

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin Sa´d as-Suhaymiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://darulhadith.com/ar-salafs-satt-med-dagens-ahl-ul-bida-olampligt/
  • Imechapishwa: 06/09/2023