Inafaa ingawa bora ni kuacha kufanya hivo

Swali: Je, inafaa kuswali Raatibah ya kabla ya Dhuhr. Je, inafaa kuswali Rak´ah zote nne kwa Tasliym moja?

Jibu: Ndio. Mchana inafaa kuswali Rak´ah zote nne pamoja kwa Tasliym moja. Kilichokatazwa ni kuswali swalah ya usiku Rak´ah nne mfululizo kwa Tasliym moja; inakuwa Rak´ah mbilimbili. Swalah ya usiku ni Rak´ah mbilimbili. Katika baadhi ya masimulizi kumetajwa hata swalah ya mchana. Bora na salama zaidi ni kuacha kufanya hivo.

Swali: Ikiwa inafaa kufanya hivo kwa Tasliym moja aifananishe na Dhuhr…

Jibu: Hapana. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kufanya hivo. Asiifananishe na Dhuhr kwa njia ya kwamba akakaa Tashahhud ya kwanza. Asifanye hivo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (35)
  • Imechapishwa: 06/09/2023