5 – Faatwimah bint Qays amesema:

”Abu ´Amr bin Hafsw alimtaliki daima[1] wakati ambapo alikuwa hayupo. Akaja kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sllam) na kumweleza hilo ambapo akamwamrisha akae eda katika nyumba ya Umm Shariyk. Baada ya kitambo akabadilisha na kusema: ”Huyo ni mwanamke anayetembelewa na wanamme[2]. Kaa eda katika nyumba ya Umm Maktuum. Ni mtu kipofu na unaweza kuzivua nguo zako nyumbani kwake. Hatokuona wakati utapovua shungi yako.” Akasema: ”Hivyo nikaenda kwake. Ilipomalizika eda yangu nilisikia wito wa mwenye kuita akisema: ”Hii ni swalah ya pamoja.” Nikaondoka kwenda msikitini na kuswali na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sllam). Ilipomalizika swalah akakaa juu ya mimbari na kusema: ”Naapa kwa Allaah! Mimi sijakukusanyeni kwa sababu ya shauku wala woga bali nimekukusanyeni kwa sababu Tamiym ad-Daariy ambaye alikuwa mnaswara amekuja, akala kiapo kwangu na akasilimu. Amenieleza kisa ambacho nilikuwa nakuelezeni kuhusu al-Masiyh ad-Dajjaal… ”[3]

Hadiyth hii imetokea mwishoni mwa uhai wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sllam), kwa sababu Tamiym ad-Daariy alisilimu mwaka wa 09. Hivyo ikafahamisha kuwa tukio hilo lilitokea baada ya Aayah ya jilbaab. Kwa msemo mwingine Hadiyth ni dalili ya wazi inayoonyesha kuwa uso sio uchi.

[1] Katika upokezi mwingine imekuja ya kwamba alimtaliki mara tatu.

[2] Katika upokezi mwingine imekuja:

”Nenda kwa Umm Shariyk ambaye alikuwa mwanamke wa tajiri wa Wanusuraji na pia ambaye alikuwa anajitolea kiasi kikubwa cha fedha katika njia ya Allaah na kwa ajili hiyo anatembelewa na wageni wengi.” Nikasema: ”Nitafanya hivo.” Ndipo akasema: ”Usifanye hivo. Umm Shariyk ni mwanamke anayetembelewa sana na wageni. Mimi sipendi ikuanguke shungi yako au nguo ifunuke kutoka miguuni mwako na watu waone kutoka kwako kile usichokipenda. Nenda kwa binamu yako kipofu ´Abdullaah bin Umm Maktuum.”

[3] Muslim (4/195-196) och (8/203).

Dalili juu ya kwamba uso sio uchi iko wazi kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimkubalia wageni wa kiume wamuone Faatwimah bint Qays hali ya kuwa na shungi. Shungi inafunika nywele kichwani peke yake. Kwa vile alikhofia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumwanguka shungi yake na kuonekane kutoka kwake kitu ambacho ni haramu kwa andiko la wazi, ndipo akamwamrisha kufanya jambo ambalo ni salama zaidi kwake ambalo ni kwenda nyumbani kwa Ibn Umm Maktuum ambaye alikuwa kipofu ambaye hawezi kumuona pindi atakapovua mtandio wake.

Kuhusu Hadiyth:

”Nyinyi pia ni vipofu?”

cheni ya wapokezi wake ni nyonge na inapingana na zilizo Swahiyh. Nimeyabainisha hayo katika ”adh-Dhwa´iyfah” (5958).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 66-67
  • Imechapishwa: 06/09/2023