14. Maswahabah wa kike hawakuwa wakitambulika kutokana na giza

4 – ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

”Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa anaswali Fajr walikuwa waumini wa kike wakiswali pamoja naye, wakijifunika nguo zao. Kisha wanarejea majumbani mwao na hakuna anayewatambua kutokana na giza.”[1]

Dalili hapa ni kwamba hawakuwa wanaweza kufahamika kutokana na giza. Maana yake ni kuwa wangefahamika kama kusingelikuwa giza. Wangelijulikana kikawaida kutokana na nyuso zao zilizofunuliwa. Hapo kumethibiti kile ninachokisema. Ijtihaad hiyo imenukuliwa na ash-Shawkaaniy (02/15) kutoka kwa al-Baajiy. Kisha baadaye nikapata upokezi mwingine unaosema wazi:

”Baadhi yetu tusingelijua nyuso za wengine.”

[1] al-Bukhaariy (372), Muslim (645) na wengineo. Nimeitaja katika ”Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (449).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 65-66
  • Imechapishwa: 06/09/2023