13. Swahabah wa kike aliyefikiriwa na Mtume

Hadiyth inatiliwa nguvu vilevile na kitendo cha wanawake wengi katika wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambao walikuwa wakionyesha uso na mikono yao mbele yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pasi na yeye kuwakemea juu ya hilo. Zipo dalili nyingi juu ya hilo. Hapa tutaorodhesha baadhi ya zile ambazo nakumbuka:

3 – Sahl bin Sa´d amesema:

”Mwanamke mmoja alikuja kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) [wakati ambapo alikuwa msikitini] akasema: ”EE Mtume Allaah! Nimekuja kujitunuku nafsi yangu kwako.” [Akanyamaza. Akabaki kitambo fulani hali ya kuwa amenyamaza] Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwangalia na kumwangalia ambapo akainamisha kichwa chake. Wakati mwanamke yule alipoona kuwa hakuvutiwa naye akaketi chini.”[1]

[1] al-Bukhaariy (9/107), Muslim (4/143), an-Nasaa’iy (2/86), Ahmad (5/330, 334 na 336), al-Humaydiy (2/414), ar-Rawayaaniy (2/69/1), Abu Ya´laa (13/514) na al-Bayhaqiy (7/84) ambaye ameipa Hadiyth kichwa cha khabari kinachosema:

”Mwanamme kumwangalia mwanamke ambaye anataka kumuoa.”

Haafidhw Ibn Hajar amesema:

”Hadiyth inajulisha kufaa kuzingatia urembo wa mwanamke kwa lengo la kutaka kumuoa. Haijalishi imetokea bila kupanga au halikutokea jambo la kumposa, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwangalia kwa kutokupanga na bila kumposa. Kisha akasema:

”Sina haja ya wanawake.”

Ingelikuwa kutafakari hakukuwa kwa lengo la kumkubali wakati wa kupendezwa naye basi kusingelikuwa na maana yoyote. Mtu anaweza kufasiri pia kwamba hilo ni jambo maalum kwake kwa sababu yeye amekingwa na kukosea. Ijtihaad yangu ni kwamba ilikuwa inafaa kwake tu kuwaangalia waumini wa kike wa kando naye, tofauti na waumini wengine. Ibn-ul-´Arabiy anayo maelezo mengine; kuna uwezekano hayo yalitokea kabla ya ulazima wa Hijaab au pia baada yake katika hali ambayo alikuwa amejifunua. Lakini kutokana na mazingira ya Hadiyth tafsiri yake iko mbali kabisa.” (Fath-ul-Baariy (9/210))

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 64-65
  • Imechapishwa: 06/09/2023