Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke kuonesha uso wake na vitanga vyake vya mikono mbele ya ndugu za mume wake wa kiume au hili ni haramu?

Jibu: Tunasema hili ni haramu. Ndugu zake mume ni kama wanaume wengine  wa kando. Si halali kwao kumtazama mke wa kaka yao. Sio halali kwake (mwanamke) kuonesha uso wake na vitanga vyake mbele yao. Kama ambavyo sio halali kwa wasiokuwa hao vilevile. Bali ndugu zake mume na jamaa zake ni khatari zaidi kuliko watu wa kando. Na kwa hili, pindi Mtume (´alayhis-Salaam) alipotahadharisha kutongia mahala walipo wanawake, akaulizwa:

“Ewe Mtume wa Allaah! Vipi kuhusu shemeji?” Akasema: “Sehemaji ni mauti.”

Bi maana ni wajibu kuwakimbia kama mauti yanavyokimbiwa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=gkbuuY3Jj4s
  • Imechapishwa: 28/01/2024