Swali: Umm ´Abdullaah anasema, anakutana na baadhi ya dada ambao wanaonyesha nyuso zao na wanatumia hoja kuwa hili lipo katika madhehebu ya Imaam ash-Shaafi´iy na madhehebu ya Hanafiy…

Jibu: Enyi ndugu zangu! Ninamuomba Allaah atupe sote tawfiyq na mafanikio. Enyi ndugu zangu! Hijaab ni tabia ya Kiislamu, jambo lililofanya mama wa waumini, Maswahabah katika zama za Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), zama za makhaliyfah waongofu na karne bora mpaka kulipokuja fikira za kimagharibi chafu. La sivyo, wake wa waumini walikuwa wakijigubika Hijaab na walikuwa wakiona Hijaab ni jambo la kiwajibu na ni tabia ya Kiislamu. Wale wanaonadi kuwa Hijaab haina asli, wanaipiga vita, kuilaumu na kuifanyia maskhara Hijaab, watu hawa wako kinyume na uongofu. Tunamuomba Allaah msimamo.

Katika baadhi ya chaneli leo kuna watu wamejitokeza na kuidhoofisha swalah ya mkunsanyiko na wanasema kuwa swalah katika misikiti haina fadhilah yoyote na wala haina maana yoyote. Swali nyumbani kwako. Wanafanya sawa swalah (za faradhi) zinazoswaliwa nyumbani na misikitini. Wanakwenda kinyume na kuivunja Sunnah ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wanailaumu Sunnah ya kuswali misikitini. Swalah ya Msikitini ina daraja ishirini na tano. Wao wanasema: “Hapana, swali nyumbani kwako au mahala popote na zote ni sawa na wala hakuna tofauti kati ya hili na hili.”

Bali baadhi yao wamepetuka mipaka na kusema, kuwaamrisha watu kuswali (misikitini) mkusanyiko ni kumwingilia mtu maisha yake binafsi. Na baadhi ya wengine wanapuuza siku ya ´Arafah na kusema kufunga siku ya ´Arafah kwa wasiokuwa wenye kuhiji haina fadhila yoyote na wala haina asli n.k. Kisha wanadai kuwa wanajua tofauti na rai mbalimbali na ni ipi yenye nguvu. Wanasema kuwa wana maoni mengi ambayo watayaeneza. Yote haya – A´udhubi Allaah – ni kupuuza kheri na madhehebu ya Salaf-us-Swaalih na maimamu wa uongofu. Ni wajibu wa chaneli zote kumcha Allaah.

Tunawanasihi wasimamizi wa chaneli wamche Allaah katika nafsi zao na wasiwawekee jamiiwatu ambao wanaiharibu dini yao na maadili yao. Na wamche Allaah katika nafsi zao. Na wasimuweke isipokuwa yule wanayejua kuwa ni wa kheri na anasifika kwa dini yake. Ama kunajitokeza watu ambao wanaponda elimu na kheri, wanaivunja misingi ya Kiislamu, mambo ya wajibu na fadhila za Kiislamu, haya yote ni makosa.

Chaneli zote natahadharisha wasiwe ni walinganizi katika upotofu. Badala yake wanatakiwa wawe ni wenye kutoa nasaha. Ama kuleta kila siku kwenye chaneli watu ambao hawamwogopi wala hawamchi Allaah. Mimi nataraji kutoka kwa ndugu zangu wawatanabahishe waislamu na wamche Allaah na watahadhari na maneno ya Allaah:

لِيَحْمِلُوا أَوْزَارَهُمْ كَامِلَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۙ وَمِنْ أَوْزَارِ الَّذِينَ يُضِلُّونَهُم بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ أَلَا سَاءَ مَا يَزِرُونَ

 “Ili wabebe mizigo [ya madhambi] yao kamili Siku ya Qiyaamah na mizigo ya wale waliowapoteza bila ya elimu – Zindukeni! Uovu ulioje wanayoyabeba!” (16:25)

“… Na yule mwenye kulingania katika upotevu, ana mzigo wa madhambi mfano wa madhambi ambayo watakayoyafanya bila ya kupunguziwa chochote katika madhambi yao.”

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=JGyonbgbjYI
  • Imechapishwa: 28/01/2024