Swali: Katika mji wetu watu wanasherehekea maulidi ya Mtume na alama ya sherehe inakuwa ni halwa na wanaiita kuwa ni “Halwa ya maulidi”. Je, inajuzu kwetu kula katika halwa hii katika wakati huu?

Jibu: Haijuzu kwenu kushiriki katika sherehe hii hata kama kutakuwa hakuna halwa. Haijuzu kwenu vilevile kula katika chakula ambacho kimeandaliwa kwa ajili yake au halwa. Kwa kuwa huku ni kujifananisha na wakristo kwa kusherehekea kwao kuzaliwa kwa al-Masiyh. Sherehe ambayo wamezusha wao na kudai. Allaah amemuweka mbali al-Masiyh na hili. Hili halijuzu.

Ni wajibu kukemea. Ni wajibu kukataza. Ni wajibu kuwabainishia watu kuwa hili halijuzu, limezushwa, ni kujifananisha na wakristo na mfano wa hayo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (01) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14301
  • Imechapishwa: 17/11/2014