Ni wajibu kuwa na utulivu katika swalah

Inashangaza kuona jinsi shaytwaan anavocheza na nwanadamu. Anasimama mbele ya Allaah (´Azza wa Jall), anamnong´oneza, anajikurubisha Kwake kwa maneno, kumsifu na kumuomba du´aa. Kisha wamuona anadonoa swalah yake kana kwamba anakimbizwa na adui. Ni kwa nini? Lau utasimama mbele ya mfalme miongoni mwa wafalme wa kidunia na huku anakunong´oneza na kukuzungumzisha, lau utabaki saa mbili unazungumza naye hilo litakuwa ni jepesi kwako. Hii ni hali ya kusimama kwa miguu yako. Hili sio kama kwenda katika Rukuu’, Sujuud na kukaa kitako. Kinyume chake utafurahi kuona mfalme huyu anazungumza na wewe hata akikaa na wewe kwa muda mrefu. Vipi tusemeje wewe huku wazungumza na Mola Wako, aliyekuumba, akakuruzuku na akakuneemesha na unadonoa namna hii? Lakini hata hivyo shaytwaan ni adui wa mwanadamu. Muumini ndiye ambaye humfanya shaytwaan kuwa ni adui. Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّ الشَّيْطَانَ لَكُمْ عَدُوٌّ فَاتَّخِذُوهُ عَدُوًّا ۚ إِنَّمَا يَدْعُو حِزْبَهُ لِيَكُونُوا مِنْ أَصْحَابِ السَّعِيرِ

“Hakika shaytwaan kwenu ni adui, hivyo basi [nyinyi] mfanyeni kuwa ni adui. Hakika anaitia kikosi chake [wanaomtii] ili wawe watu wa Motouwakao kwa nguvu.” (35:06)

Ni wajibu kwa mwanadamu kuwa na utulivu katika swalah yake. Kuonekane utulivu kwake katika swalah yake yote na maneno yake [ya ndani ya swalah].

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/400-401)
  • Imechapishwa: 04/06/2023