14. Mlinganizi anapata mfano wa thawabu za aliyemlingania

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhiwa sallam) amesema katika Hadiyth Swahiyh:

“Yeyote anayejulisha katika jambo basi ana ujira wa mfano wa mtendaji.”[1]

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

Vilevile amesema tena (Swalla Allaahu ´alayhiwa sallam):

“Yeyote anayelingania katika uongofu basi anapata ujira mfano wa yule mwenye kumfuata pasi na kupungua chochote katika ujira wao. Na yeyote anayelingania katika upotevu basi anapata dhambi mfano wa yule mwenye kumfuata pasi na kupungua chochote katika dhambi zao.”[2]

Hapa kuna fadhilah za kulingania katika dini ya Allaah (´Azza wa Jall).

[1] Muslim (1893).

[2] Muslim (2674).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Da´wah ilaa Allaah wa Akhlaaq-id-Du´aah, uk. 23-24
  • Imechapishwa: 04/06/2023