13. Mtume na wafuasi wake wanalingania kwa elimu

Miongoni mwazo ni maneno Yake (´Azza wa Jall):

قُلْ هَـٰذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّـهِ ۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ اتَّبَعَنِي

“Sema: “Hii ndio njia yangu: nalingania kwa Allaah, juu ya ujuzi na umaizi – mimi na anayenifuata.”[1]

Akabainisha (Subhaanah) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhiwa sallam) analingania kwa utambuzi na kwamba vivyo hivo ndio hali ya wafuasi wake. Hapa kuna fadhilah za ulinganizi na kwamba wafuasi wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhiwa sallam) ndio wanaolingania katika njia yake kwa utambuzi. Utambuzi (البصير) ni ile elimu ya yale anayoyalingania na anayoyakataza. Hapa kuna utukufu na ubora wao.

[1] 12:108

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Da´wah ilaa Allaah wa Akhlaaq-id-Du´aah, uk. 23
  • Imechapishwa: 04/06/2023