Ni upi muda mchache kabisa na mwingi wa I´tikaaf?

Swali: Ni upi muda mchache kabisa na mwingi wa I´tikaaf?

Jibu: Haina mpaka maalum. I´tikaaf haina mpaka maalum wa siku, muda wake mchache au saa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuweka mpaka wa chochote. Allaah hakuweka mpaka wa chochote. Hapana vibaya mtu akiingia msikitini na akanuia kukaa I´tikaaf saa moja, siku moja au siku mbili. Haina kikomo maalum. Hakika mambo yalivyo ni kwamba mtu anaifanya kwa ajili ya kujikurubisha kwa Allaah, kujishughulisha na ´ibaadah, kusoma Qur-aan ndani ya Ramadhaan na aina nyenginezo za ´ibaadah. Kwa hivyo haina mpaka maalum. Kwa mujibu wa maoni sahihi si sharti mtu awe amefunga ili aweze kukaa I´tikaaf. Bali inafaa mtu akakaa I´tikaaf hata kama hakufunga. Hivo ndivo alivosema Ibn ´Abbaas na wengineo (Radhiya Allaahu ´anhum) kwamba haina kikomo maalum. ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) alisema:

“Ee Mtume wa Allaah! Mimi niliweka nadhiri ya kukaa I´tikaaf usiku mmoja ndani ya msikiti Mtakatifu.” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Tekeleza nadhiri yako.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/audios/794/فتاوى-رمضانية
  • Imechapishwa: 15/04/2023