Namna ya kuweka nia ya kuingia katika I´tikaaf

Swali: Ni vipi kuweka nia kwa ambaye anataka kukaa I´tikaaf mwezi wa Ramadhaan siku tano  au siku kadhaa?

Jibu: I´tikaaf haina kikomo maalum. Lakini bora ni kufanya I´tikaaf yale masiku kumi ya mwisho. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akikaa I´tikaaf yale masiku kumi ya mwisho yote. Hapana vibaya mtu akikaa I´tikaaf siku moja au mbili. Jambo ni lenye wasaa. Ataweka nia ya kukaa msikiti kwa ajili ya kuleta Dhikr, kusoma Qur-aan, kuswali na kadhalika katika yale masiku kumi ya mwisho, katika yale masiku ishirini ya mwanzo au katika miezi mingine isiyokuwa Ramadhaan. Jambo ni lenye wasaa. I´tikaaf inapendeza Ramadhaan na miezi mingine ingawa ndani ya Ramadhaan ndio bora zaidi na kumekokotezwa zaidi na khaswakhaswa katika yale masiku kumi ya mwisho.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/audios/794/فتاوى-رمضانية
  • Imechapishwa: 15/04/2023