13. Kuhukumiana kwa sheria zinazotunga watu

Haijuzu kuhukumiwa kwa kanuni hata kama utakuwa unaitakidi kuwa hukumu ya Shari´ah ndio bora zaidi. Katika hali hii utakuwa umehalalisha jambo ambalo kilazima linajulikana kidini uharamu wake. Ni kama mfano wa mwenye kusema zinaa ni halali lakini hata hivyo mimi sizini au akaona kuwa ribaa ni halali lakini mimi sintokula ribaa, huyu anakufuru. Kwa sababu ribaa ni haramu. Kule kuihalalisha ilihali ni jambo ambalo kilazima inajulikana kidini uharamu wake ni kufuru.

Vilevile ikiwa ataona kuwa hukumu ya kanuni inafaa ingawa hukumu ya Shari´ah ndio bora zaidi. Kile kitendo cha kujuzisha kwako hukumu ya kanuni ni kufuru na kuritadi. Kwa sababu umehalalisha jambo la haramu ambalo inajulikana kilazima katika dini uharamu wake. Kuhukumu kwa kanuni ni haramu kwa maafikiano. Ni kama mfano wa zinaa ambayo ni haramu kwa maafikiano. Ni kama mfano vilevile wa ribaa ambayo ni haramu kwa maafikiano. Kwa hivyo yule mwenye kusema kuwa zinaa ni halali anakufuru. Mwenye kusema ribaa ni halali anakufuru. Mwenye kusema inajuzu kuhukumu kwa kanuni anakufuru. Haijalishi kitu hata kama atakuwa anaitakidi kuhukumu kwa Shari´ah ndio bora zaidi.

Yule anayeamini kuwa kuna uongofu bora zaidi kuliko uongofu wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), uongofu wenye kulingana nao au usiyolingana nao sambamba na hilo akaona kujuzu kufuata uongofu mwingine usiokuwa wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi anakufuru.

Vivyo hivyo yule mwenye kuamini ya kwamba inajuzu kuhukumu kinyume na hukumu ya Allaah na Mtume Wake – ni mamoja ikiwa ataamini kuwa hukumu ya Allaah ndio bora zaidi, iko chini zaidi au inalingana nayo – anakuwa kafiri. Si kwa jengine bali ni kwa sababu amehalalisha jambo ambalo inajulikana kilazima katika dini uharamu wake. Dalili ni kuwa hakushuhudia ya kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah. Ambaye hakushuhudia ya kuwa Muhammad ni Mtume wa Allaah anakuwa kafiri. Kushuhudia ya kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah kunapelekea kuhukumu kwa Shari´ah yake na kuitakidi kuwa haijuzu kuhukumiana kwa isiyokuwa Shari´ah yake na vilevile kuamini kuwa haijuzu kufuata uongofu usiokuwa wa uongofu wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tabswiyr-ul-Anaam bisharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 30-31
  • Imechapishwa: 15/04/2023