Anataka kukata I´tikaaf na badala yake kufanya ´Umrah

Swali: Kuna mtu yuko I´tikaaf na anataka kumfanyia ´Umrah baba yake. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Ikiwa I´tikaaf yake imewekewa nadhiri na kikomo kwa muda maalum, basi analazimika kukamilisha I´tikaaf yake. Kwa sababu ni lazima kutimiza nadhiri ya utiifu. Na kama I´tikaaf yake ni ya kujitolea tu, basi akitaka ataikamilisha, na akitaka ataikata na kufanya ´Umrah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/446)
  • Imechapishwa: 15/04/2023