Ni swalah zipi zilizokatazwa kuziswali makaburini?

Swali: Hadiyth inakataza kuswali kati ya makaburi. Nini maana yake? Watu huswali swalah yaj jeneza kati ya makaburi pindi inapowapita misikitini.

Jibu: Hadiyth inakusudia swalah zingine zote isiyokuwa swalah ya jeneza. Haina neno kuswali swalah ya jeneza kati ya makaburi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswali swalah ya jeneza juu ya yule bwana ambaye alikufa ambaye alikuwa akiusafisha msikiti. Isitoshe makatazo ya kuswali makaburini kwa sababu ya kuogopa mtihani na kuwashirikisha wale wafu, jambo ambalo liko mbali kabisa juu ya ile swalah ya jeneza.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/377)
  • Imechapishwa: 02/05/2026