Swali: Ni ipi hukumu ya kutundika picha kwenye ukuta?

Jibu: Ni haramu, khaswa zile picha kubwa, hata kama hakuonekani isipokuwa tu sehemu ya mwili au kichwa. Lengo la kutukuza picha hizi liko wazi. Msingi wa shirki ni kupetuka mipaka huku. Imesihi kupokelewa kupitia kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ambaye amesema kuhusiana na maneno ya Allaah (Ta´ala):

وَقَالُوا لَا تَذَرُنَّ آلِهَتَكُمْ وَلَا تَذَرُنَّ وَدًّا وَلَا سُوَاعًا وَلَا يَغُوثَ وَيَعُوقَ وَنَسْرًا

”Wakasema: “Msiwaache waungu wenu – na wala msimwache Wadd na wala Suwaa´ na wala Yaghuuth na Ya’uuq na Nasr!”[1]

“Haya ni majina ya waja wema katika watu wa Nuuh. Walipokufa shaytwaan aliwapendezea watu wake watengeneze masanamu na kuyaweka mahali ambapo walikuwa wakikaa na kuyapa majina yao. Wakafanya hivyo na hawakuyaabudu mpaka walipofariki watu wale na elimu ikasahaulika, hivy ndipo wakaabudiwa.”[2]

[1] 71:23

[2] al-Bukhaariy.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/342-343)
  • Imechapishwa: 02/05/2026