Ni Sunnah kuleta du´aa ya kufungulia swalah na Isti´aadhah katika swalah ya jeneza?

Swali: Du´aa ya kufungulia swalah imewekwa katika Shari´ah kuisoma katika swalah ya jeneza? Je, mtu alete Isti´aadhah kabla ya kuanza kisomo?

Jibu: Wanachuoni wamesema kuwa haikupendekezwa na wakasema ni kwa sababu ya kwamba swalah ya jeneza imejengwa juu ya ukhafifishaji. Ikiwa imejengwa juu ya ukhafifishaji basi kutakuwa hakuna du´aa ya kufungulia swalah.

Kuhusu kuleta Isti´aadhah afanye hivo kwa kuwa atasoma Qur-aan. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَإِذَا قَرَأْتَ الْقُرْآنَ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ

“Unapotaka kusoma Qur-aan basi, omba ulinzi kwa Allaah kutokamana na shaytwaan aliyefukuzwa mbali.”[1]

[1] 16:98

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/119)
  • Imechapishwa: 07/09/2021