Ni ipi hukumu ya kusoma Suurah nyingine baada ya al-Faatihah?

Swali: Ni ipi hukumu ya kusoma Aayah baada ya al-Faatihah katika swalah ya jeneza?

Jibu: Ni sawa kwa mtu akasoma katika swalah ya jeneza sehemu kidogo katika Qur-aan baada ya al-Faatihah. Akisoma al-Faatihah peke yake ni sawa kwa kuwa swalah ya jeneza imejengwa juu ya ukhafifishaji. Kwa ajili hii ndio maana du´aa ya kufungulia swalah haikuwekwa katika Shari´ah. Alete Isti´aadhah kisha asome al-Faatihah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/121)
  • Imechapishwa: 07/09/2021