115. Salaf wanatakiwa kupendwa na kufatwa

Miongoni mwa haki ya Salaf juu yetu ni sisi kuwaombea msamaha. Allaah (Ta´ala) amesema kuhusu Wahajiri na Wasaidizi:

لِلْفُقَرَاءِ الْمُهَاجِرِينَ الَّذِينَ أُخْرِجُوا مِن دِيَارِهِمْ وَأَمْوَالِهِمْ يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانًا وَيَنصُرُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ وَالَّذِينَ تَبَوَّءُوا الدَّارَ وَالْإِيمَانَ مِن قَبْلِهِمْ يُحِبُّونَ مَنْ هَاجَرَ إِلَيْهِمْ وَلَا يَجِدُونَ فِي صُدُورِهِمْ حَاجَةً مِّمَّا أُوتُوا وَيُؤْثِرُونَ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ ۚ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ وَالَّذِينَ جَاءُوا مِن بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ

“Wapatiwe pia mafuqara Muhaajiruun ambao wametolewa kutoka majumbani mwao na mali zao wanatafuta fadhilah na radhi kutoka kwa Allaah na wanamnusuru Allaah na Mtume Wake – hao ndio wakweli. Na wale waliokuwa na makazi [Madiynah] na wakawa na imani kabla yao wanawapenda wale waliohajiri kwao na wala hawahisi choyo yoyote vifuani mwao kwa yale waliyopewa [Muhaajiruun] na wanawapendelea kuliko nafsi zao japokuwa wao wenyewe ni wahitaji. Na yeyote anayeepushwa na uchu wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu.” Na wale waliokuja baada yao wanasema: Rabb wetu! Tughufurie na ndugu zetu ambao wametutangulia kwa iymaan na wala Usijaalie katika nyoyo zetu mafundo ya chuki kwa wale walioamini; Rabb wetu! Hakika Wewe ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu.”[1]

Hawakutosheka kuwaombea msamaha ndugu zao isipokuwa wameomba pia wasalimishwe kutokamana na bughudha na chuki dhidi yao. Kwa ajili hiyo Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Miongoni mwa misingi ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni wenye mioyo na ndimi zilizosalimika juu ya Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

Nyoyo zao ni zenye kusalimika kutokamana na bughudha na chuki. Kwa sababu yule ambaye anamchukia Swahabah ni mnafiki na sio muumini. Maswahabah hawatakiwi kusemwa vibaya wala kupunguzwa hadhi zao na wala haifai kwa yeyote kutafuta makosa yao. Bali wanapaswa kuombewa Allaah awasamehe na awawie radhi, wanawapenda na kuwafuata. Namna hii ndivo ulivyo mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah pamoja na Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam); kuwaigiliza na kufuata mfumo wao na ni wenye mioyo iliosalimika kutokamana na kuwachukia na ndimi zilizosalimika kutokamana na kumtukana yeyote katika wao. Huu ndio mfumo wa Qur-aan na Sunnah na mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Usahihi haufikiwi kwa njia nyingine. Wale waliokuja nyuma wakiwadharau watangu wao na wakawarushia ujinga, upumbavu na mfano wa hayo si jengine isipookuwa ni upotofu na kutoshikamana na Qur-aan na Sunnah. Kwa sababu Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّـهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا

“Shikamaneni kwa kamba ya Allaah nyote pamoja wala msifarikiane.”[2]

Ummah mzima wanatakiwa kushikamana na kamba ya Allaah, ambayo ni Qur-aan na Sunnah, na wala wasifarikiane.

[1] 59:08-09

[2] 03:103

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 88-89
  • Imechapishwa: 07/09/2021