“Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Dini iliyojengeka katika imani ya moyo (elimu yake na hali yake) ndio msingi na matendo yaliyodhahiri ndio matawi na ukamilifu wa imani.”

Ibn Taymiyyah anachokusudia ni kwamba dini inayo msingi na tanzu, na makusudio yake si kwamba matendo ni sharti ya kutimia na tanzu ya imani. Murji-ah wa leo ndio wenye kuona kuwa mwenye kuacha matendo bado imani yake inabaki na yenye kusihi.”[1]

Shaykh-ul-Islaam amebainisha wazi ya kwamba imani ni msingi na kwamba yale matendo yanayodhihiri ndio matawi yake na utimilifu wake. Amesema waziwazi ya kwamba dini imejengeka katika imani ya moyo (elimu yake na hali yake). Ndipo anakuja mtu wa batili huyu mwongo na kujaribu kuyapindisha maana maneno haya ya Ibn Taymiyyah yaliyo wazi na kusema:

“Ibn Taymiyyah anachokusudia ni kwamba dini inayo msingi na tanzu, na makusudio yake si kwamba matendo ni sharti ya kutimia na tanzu ya imani. Murji-ah wa leo ndio wenye kuona kuwa mwenye kuacha matendo bado imani yake inabaki na yenye kusihi. Ibn Taymiyyah hakukusudia hivo.”

Ni nani aliyesema kuwa Ibn Taymiyyah amesema kuwa matendo ni sharti ya kutimia kwa imani? Nimesema hivo? Je, ndugu zangu kama vile Shaykh Ahmad an-Najmiy, Shaykh Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy, Shaykh Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy, Shaykh ´Ubayd, Shaykh Swaalih as-Suhaymiy au Salafiy mwingine Makkah au Madiynah aliwahi kusema kuwa imani ni sharti ya kutimia kwa imani? Bainisha maneno hayo kupitia vitabu vyao, kanda zao na darsa zao.

[1] al-Burkaan, uk. 17

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kashf Akaadhiyb wa Tahriyfaat wa Khiyaanaat Fawziy al-Bahrayniy, uk. 160-161
  • Imechapishwa: 06/08/2023