al-Bahrayniy amesema baada ya uwongo wake uliyotangulia:

“Rabiy´ ndiye anayesema kuwa matendo ni sharti ya kutimia kwa imani.”[1]

Haya ni katika uwongo na uzushi wake mkubwa. Mimi ni miongoni mwa watu wa mwanzo waliyokemea na kukaripia nadharia hiyo, na bado nafanya hivo mpaka sasa mpaka kesho – Allaah akitaka. Nimemraddi kwa uwongo huo mara nyingi. Miongoni mwa matahadharisho yangu juu ya nadharia hiyo ni pamoja na:

“Allaah anajua kuwa mimi ni miongoni mwa watu wa mwanzo waliyotahadharisha nadharia hiyo kabla ya kutoka kitabu cha Khaalid al-´Anbariy. Nilimtahadharisha al-´Anbariy na kumuomba ayaondoshe maudhui hayo kutoka kwenye kitabu. Wakati tasnifu hiyo baadaye ilipokuwa mada yenye kuzungumzwa, nikatadharisha kuitumia au kuipekua ndani yake. Badala yake niliwahimiza wote wanaozungumzia imani kushikamana na utambulisho wa Salaf juu ya imani. Kutokana na ninavojua Faalih hakusema chochote juu ya jambo hilo kipindi hicho. Hivi sasa ndipo ameanza kuzungumza kwa ajili ya kuchokoza, kutahini na kufanya Tabdiy´ kwa uwongo na uvumi[2].”

Nilimwambia Faalih katika makala ”Kalimah fiyt-Tawhiyd”:

“Wanabadilikabadilika rangi kama kinyonga juu al-Albaaniy na mada nyenginezo. Hatimaye wanatangaza wazi ya kwamba Rabiy´ amemfuata kichwa mchunga al-Albaaniy katika suala la imani na kwamba matendo ni sharti ya kutimia kwa imani. Naapa kwa Allaah ya kwamba mimi nilipiga vita msemo unaosema kuwa “matendo ni sharti ya kutimia kwa imani” na bado nafanya hivo. Nadhani kuwa hayo yalikuwa mwaka wa 1415 ambapo niliyakaripia. Tangu kipindi hicho nilimkemea kutumia msemo huo na kumwambia:

“Huu ndio utambulisho wa Ahl-us-Sunnah. Lazimiana na utambulisho wa Ahl-us-Sunnah juu ya imani. Utambulisho wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah juu ya imani ni kwamba ni: maneno, matendo na kuamini; inazidi kwa utiifu na inashuka kwa maasi.”[3]

[1] al-Burkaan, uk. 39

[2] Tazama ”al-Majmuu´ al-Waadhwih”, uk. 367

[3] Tazama ”al-Majmuu´ al-Waadhwih”, uk. 504

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kashf Akaadhiyb wa Tahriyfaat wa Khiyaanaat Fawziy al-Bahrayniy, uk. 213-214
  • Imechapishwa: 06/08/2023