297 – Ibn Abiy Maryam amenihadithia, kutoka kwa Muhammad bin ´Abdil-´Aziyz: Mama yangu amenihadithia:

”Siku moja baba yako alinambia: ”Natamani maziwa kwa mkate mnene.” Nikamwandalia kwa ajili ya futari yake na kumwelekea mbele yake. Tahamaki akaja mwombaji na kusema: ”Ni nani atakayemkopesha Tajiri, Mwaminifu?” Baba yako akasema: ”Mja wake asiyekuwa na matendo mema.” Akatoka nje ya lile bakuli na kumpa yule mwombaji. Akalala usiku hali ya kuwa na njaa. Nikamwambia kabla ya kupambazuka: ”Nisikupe kipande cha mkate, ili angalau kesho uweze kunyoosha mgongo wako?” Akasema: ”Hapana. Sihitaji.”

298 – Ibn Abiy Maryam amenihadithia, kutoka kwa Qabiyswah: Mmoja katika marafiki zangu amenihadithia:

”Mwanamke mmoja katika kutoka katika familia ya Daawuud at-Twaa-iy alimtengenezea Daawuud at-Twaa-iy malai ya siagi. Wakati ilipofika wakati wa kukata swawm, akamtumia nayo pamoja mjakazi wake. Kulikuwa na mafungamano ya kunyonya kati ya mwanamke huyo na wao. Mjakazi yule akasema: ”Nikamwendea na bakuli na kuliweka mbele yake kwenye chumba. Pindi alipokuwa anajiandaa kuanza kula akaja mwombaji na kusimama mlangoni. Akasimama kwa ajili yake na kumpa nayo, ambapo akakaa pamoja naye nje ya mlango mpaka alipomaliza kula. Kisha akaingia ndani. Akaosha bakuli lile na kuzielekea tende zilizokuwa mbele yake. Nilikuwa nafikiria kuwa amejiandalia nazo kwa ajili ya chakula chake cha jioni, lakini akaziweka tende zile kwenye bakuli, akanipa nazo na kusema: ”Mfikishie salamu.” Amempa mwombaji kile tulichomletea na ametupa kile tulichokuwa tunataka kufuturia. Nadhani kuwa hakulala isipokuwa akiwa na njaa.” Qabiyswah akasema: ”Alikuwa mwembamba sana.”

299 – Abu Sa´iyd al-Ashajj amenihadithia: ´Abdullaah bin ´Abdil-Kariym bin Hassaan, kutoka kwa Hammaad bin Abiy Haniyfah, ambaye amesimulia:

”Kuna mwanamke mmoja alikuwa akimhudumia Daawuud at-Twaa-iy. Akamwambia: ”Unasemaje nikupikie malai?” Akasema: ”Napenda.” Akampikia malai na akaja nayo, ambapo akamwambia mwanamke yule: ”Vipi kuhusu wale mayatima ya fulani?” Akasema: ”Wako kama walivyo.” Akasema: ”Wapelekee nayo.” Mwanamke yule akasema: ”Niitoe fidia nafsi yako! Hujala kitu chakula hicho kitambo fulani.” Akasema: ”Wao wakikila, basi itakuwa ni thawabu mbele ya Allaah. Na nikikila mimi, kitaingia msalani.”  

300 – Abu Sa´iyd amenihadithia: ´Abdullaah bin ´Abdil-Kariym ametuhadithia, kutoka kwa Hammaad bin Abiy Haniyfah, aliyesema:

”Niliingia kwa Daawuud at-Twaa-iy. Alikuwa amevaa nguo zilizopasukapasuka. Nikamsikia akisema: ”Nimetamani njugu, na nikakupa ukala. Kisha hivi sasa unatamani njugu na tende. Napambana usizile tena kamwe.” Nikatoa salamu na kuingia ndani. Alikuwa peke yake. Akiikosoa nafsi yake.”

301 – Muhammad bin Haaruun amenihadithia: Nimemsikia Abu Swaalih al-Farraa’ akisema: Nimemsikia Abiy Ishaaq al-Fizaariy: Nimemsikia Ibraahiym bin Ad-ham akisema:

”Tulipatwa na njaa Makkah. Kwa masiku kadhaa nikawa nalowesha udongo kwa maji ili nipate kuula.”

302 – Muhammad bin Haaruun amenihadithia: Abu ´Umayr bin an-Nahhaas ametuhadithia: Dhwamrah ametuhadithia, kutoka kwa Ibraahiym bin Ad-ham, aliyesema:

”Sioni kuwa nalipwa thawabu kwa kuacha chakula kizuri na kinywaji. Kwani mimi sikitamani.”

303 – Muhammad bin Haaruun amenihadithia: Abu Swaalih al-Farraa’ ametuhadithia: Nimemsikia Abiy Ishaaq al-Fizaariy:

”Nilisema kumwambia Ibraahiym Ad-ham: ”Sikuoni ukiburudika na anasa zao au ukila katika nyama zao. Ni kwa nini unaviacha ilihali unavihitaji?” Akasema: ”Siviachi isipokuwa ni kwa sababu sivihitaji.”

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Juu´, uk. 177-181
  • Imechapishwa: 07/08/2023