304 – ´Aliy bin Harb at-Twaa-iy ametuhadithia: Abu Daawuud al-Maghribiy ametuhadithia, kutoka kwa Ibn-us-Sammaak, kutoka kwa Ash´ath, ambaye amesema:

”Niliingia kwa Yaziyd ar-Raqaashiy, aliyesema: ”Ee Ash´ath, njoo, na ili tulie juu ya maji ya baridi kisha na baadaye tuhisi njaa.” Akaanza kusema: ”Wamenitangulia wafanya ´ibaadah na mimi nimedumaa. Masikini mimi!” Alikuwa amefunga miaka arobaini.”

305 – ´Ubaydullaah al-´Atakiy amenihadithia: Muhammad bin ´Amr ametuhadithia: Muhammad bin Marwaan ametuhadithia, kutoka kwa Yuunus bin Abiyl-Furaat, aliyesema:

”Yaziyd ar-Raqaashiy alimwandikia Ash´ath al-Haddaaniy: ”Ikiwa umekaa chini, basi simama. Na ikiwa umesimama, njoo.” Nikampanda punda na kumwendea. Nilipoingia kwake, akasema: ”Unajua ni kwa nini nimekutumia mjumbe?” Nikasema: ”Hapana.” Akasema: ”Nimekutumia ujumbe ili tupate kulia kwa ajili ya maji ya baridi siku ya Qiyaamah.”

306 – Ametuhadithia kwa kutusomea: al-Hasan bin as-Swabbaah amenihadithia: Yaziyd bin Haaruun ametuhadithia: al-Mas´uudiy ametukhabarisha, kutoka kwa ´Awn, ambaye amesema:

”Wana wa israaiyl walikuwa na msimamizi anayewaambia: ”Msile sana, kwani mkila sana basi mtalala sana. Mkilala sana, basi mtaswali kidogo.”

307 – Ya´quub bin ´Ubayd amenihadithia: Yaziyd bin Haaruun amenikhabarisha: al-Jarraah bin al-Minhaa al-Jazariy ametukhabarisha, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa bwana mmoja, kutoka kwa Ibn ´Umar, aliyesema:

”Nilitoka pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mpaka tukaingia kwenye bustani la mmoja katika Answaar. Akaanza kuokota na kula na kusema: ”Ee mwana wa ´Umar, ni kwa nini huli?” Akasema: ”Ee Mtume wa Allaah, sikitamani.” Ndipo akasema: ”Mimi nakitamani. Hii ni asubuhi ya nne ambayo sijala kitu na hata sikipati. Lau ningelitaka, basi ningelimuomba Mola wangu, na Angelinipa mfano wa Kisraa na Qayswara. Utafanya nini, ee mwana wa ´Umar, pale utapokutana na watu wanaohifadhi chakula cha mwaka mzima?” Naapa kwa Allaah! Tahamaki kukateremka:

وَكَأَيِّن مِّن دَابَّةٍ لَّا تَحْمِلُ رِزْقَهَا اللَّـهُ يَرْزُقُهَا وَإِيَّاكُمْ ۚ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ

”Viumbe wangapi hawabebi riziki zao; Allaah huwaruzuku wao na nyinyi. Naye ndiye Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa kila kitu.”[1]

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Hakika Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) hakuniamrisha kukusanya hazina ya dunia wala kufuata matamanio. Yule anayehifadhi hazina za dunia kwa kutaka maisha ya milele, basi anatakiwa kutambua kuwa uhai uko mikononi mwa Allaah. Mimi sihifadhi dinari wala diramu. Wala sihifadhi chakula kwa ajili ya siku ya kesho.”[2]

308 – al-´Abbaas bin Ja´far amenihadithia: Muhammad bin as-Swalt ametuhadithia: Abu Kudaydah ametuhadithia, kutoka kwa Layth: Mujaahid amesema:

”Ningekuwa nakula kila ninachokitamani, basi nisingestahili hata govi.”

[1] 29:60

[2] Ibn Kathiyr amesema:

”Hadiyth ni geni. Isitoshe Abul-´Utuuf al-Jazariy alikuwa dhaifu.” (Tafsiyr-ul-Qur-aan al-´Adhwiym (3/553))

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Juu´, uk. 181-184
  • Imechapishwa: 07/08/2023