52. Harufu nzuri kabisa na harufu ya mvundo siku ya Qiyaamah

309 – Muhammad bin Ishaaq ametuhadithia: Hassaan bin ´Abdillaah ametuhadithia: as-Sariy bin Yahyaa ametuhadithia, kutoka kwa Farqad as-Sabkhiy, ambaye amesema:

” Sulaymaan bin Daawuud (Swalla Allaahu ´alayhimaa wa sallam) alikuwa akiwaalika watu mkate wa ngano ilihali yeye anakula mkate wa shayiri.”

310 – Muhammad bin Ishaaq amenihadithia: Hassaan bin ´Abdillaah ametuhadithia: as-Sariy bin Yahyaa amenihadithia, kutoka kwa al-Hasan, ambaye amesema:

”Luqmaan alisema kumwambia mwanawe: ”Ee mwangu kipenzi! Usile wakati umeshashiba. Kwa sababu pengine kula huko kukaleta maradhi.”

311 – al-Hasan bin ´Abdil-´Aziyz amenihadithia: al-Haarith bin Miskiyn ametuhadithia: ´Abdullaah bin Wahb ametukhabarisha: ´Abdur-Rahmaan bin Zayd bin Aslam ametuhadithia:

”Ibn ´Umar alisuhubiana na bwana mmoja safarini. Ilikuwa wakati bwana huyo anapoalikwa chakula, basi hula tonge moja kisha akafuta mikono yake, na anapopewa kinywaji, basi anakunywa glasi moja peke yake. Ibn ´Umar akamwambia: ”Ee mtoto wa ndugu yangu kipenzi! Ni kwa nini huli chakula ukashiba? Ni kwa nini hunywi kinywaji ukakata kiu chako?” Akasema: ”Ee mwana wa ´Umar! Mbele yangu kuna moto. Naapa kwa Allaah mpaka hiyo kesho nijue pale nitapokuwa na mahali kwangu patakuwa wapi!” Baada ya mtu huyo sikumuona Ibn ´Umar akila kushiba mpaka alipoaga dunia.”

312 – Abu ´Abdillaah anilisomea mashairi: [tupu]

313 – [tupu] … harufu nzuri zaidi tangu tulipoingia Peponi kuliko hii.” Kukasemwa: ”Hii ni harufu ya vinywa vya watu waliofunga.” Watu wa Motoni watasikia harufu, ambapo waseme: ”Hatujawahi kusikia harufu mbaya zaidi kushinda hii.” Ndipo kutasemwa: ”Huu ni uvundo kunatoka kwenye tupu za makahaba.”

314 – Muhammad bin al-Husayn ametuhadithia: Yahyaa bin ´Iysaa ametuhadithia, kutoka kwa Bishr bin Mansuur, kutoka kwa Thawr bin Yaziyd, ambaye ameeleza:

”Nilisoma kwenye baadhi ya vitabu: ”Pepo kwa wale wanaohisi kiu na njaa kwa ajili ya wema. Hao ndio wale wataokaoingia kwenye ufalme Wangu wa mbinguni.”

315 – Muhammad amesema: Ishaaq bin Mansuur ametuhadithia: Abu Ishaaq al-Humaysiy ametuhadithia: Nimemsikia Yaziyd ar-Raqaashiy akisema:

”Tumefikiwa na khabari kuwa wale wanaohisi njaa kwa ajili ya Allaah watakuwa katika ngazi za kwanza siku ya Qiyaamah.”

316 – Muhammad amesema: Muhammad bin Sinaan al-Baahiliy ametuhadithia: Nimemsikia ´Abdul-Waahid bin Zayd, aliyesema:

”al-Hasan alialikwa chakula na akasema: ”Nimefunga.” Akaambiwa: ”Unafunga kwenye joto hili kali?” Akasema: ”Mimi napenda niweze kusimama kwenye zile ngazi za kwanza.”

317 – Muhammad amesema: Khaalid bin Khidaash amenihadithia: Baba yangu amenihadithia: Farqad as-Sabkhiy amesema:

”Nimesoma katika baadhi ya vitabu: ”Pepo kwa wale wanaohisi njaa kwa ajili ya Allaah. Hao ndio watakaotukuzwa katika uwanja wa mkusanyiko siku ya Qiyaamah.”

318 – Yahyaa bin Ma´iyn amesema: Sa´iyd bin al-´Aasw amesema:

Tumbo langu ni mtumwa wa heshima yangu – sio heshima yangu

likitamani chakula na mtumwa wa tumbo langu

319 – Muusa bin ´Imraan ametuhadithia: Nimemsikia Abu Sulaymaan ad-Daaraaniy akisema:

”Nafsi inapohisi njaa na kiu, basi moyo unasafika na kuwa laini. Na unaposhiba na kuhisi kiu, moyo unapofoka na kufa.”

320 – Abu ´Amr ametuhadithia: ´Abdur-Rahmaan bin Muhammad ametuhadithia, kutoka kwa Ahmad bin Abiyl-Hawaariy: Nimemsikia ´Abdul-´Aziyz bin ´Umayr akisema:

”Kundi la ndege lilihisi njaa kwa asubuhi arobaini. Waliporuka angani kwenda kwa ndugu wengine, wakarudi wakiwa na harufu ya miski.”

Mwisho

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Juu´, uk. 184-188
  • Imechapishwa: 07/08/2023