Tazama jinsi Sahl bin al-Mutawwakil anavosema:

“Nimekutana na wanazuoni elfu moja na wote wanasema: “Imani ni maneno na matendo. Inazidi na kushuka.”

Tazama jinsi al-Laalakaa’iy alivyopanga majina yao wote mmoja baada ya mwingine ambao Haddaadiyyah wote kwa pamoja hawafikii hata nyayo za miguu yao. Wamesema:

“Imani inaongezeka na kushuka.”

Hawakutaja sharti ambayo Haddaadiyyah waliochupa mipaka na waongo wameweka katika kuwapiga vita Ahl-us-Sunnah. Imaam al-Laalakaa´iy amepokea kwa cheni yake ya wapokezi ya kwamba Imaam al-Bukhaariy amesema:

“Nimeandika kutoka kwa wanazuoni zaidi ya 1000 na sikuandika isipokuwa kutoka kwa anayesema: “Imani ni maneno na matendo.” Sikuandika kutoka kwa ambaye anasema: “Imani ni maneno.”[1]

Ole wake al-Bukhaariy na waalimu wake kutokana na dhuluma ya Haddaadiyyah! Ni vipi wanaweza kusema kuwa imani ni maneno na matendo na wasizidishe inazidi na kushuka mpaka hakubaki chochote?

Kwa mujibu wa Haddaadiyyah wote kwa jumla na khaswa Faalih na Fawziy al-Bukhaariy ni Murji-ah waliopindukia. Kwa sababu wameenda kinyume na sharti ya Haddaadiyyah na yale wanayoyawajibisha kwamba ni lazima kusema kuwa imani inazidi na kupungua mpaka hakubaki chochote.

[1] Sharh Usuwl I´tiqaad Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah (5/959).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kashf Akaadhiyb wa Tahriyfaat wa Khiyaanaat Fawziy al-Bahrayniy, uk. 66-67
  • Imechapishwa: 07/08/2023