Swali: Je, mtu arejeshe swadaqah yake akimpa mtu kisha baadaye ikabainika kuwa ni tajiri?

Jibu: Haidhuru ikiwa udhahiri wake ni masikini. Ikiwa udhahiri wake ni masikini na anafanana na masikini na akafikiria kuwa ni masikini ambapo akampa, wanazuoni wanaona kuwa swadaqah yake ni yenye kusihi. Dhambi anapata mtu huyo.

Swali: Je, anapata dhambi yule ambaye hakutoa swadaqah?

Jibu: Ikiwa ni zakaah anapata dhambi. Lakini hapati dhambi ikiwa sio zakaah. Isipokuwa ikibidi. Isipokuwa pale ambapo masikini anakuwa hana njia nyingine. katika hali hiyo analazimika kumuokoa. Kilicho cha lazima ni zakaah. Kuhusu misaada mingine inategemea na sababu. Swadaqah zingine itategemea na sababu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22727/هل-لمن-تصدق-على-غني-ان-يسترد-صدقته
  • Imechapishwa: 07/08/2023