Ni muda kiasi gani inatakiwa kubaki makaburini baada ya mazishi?

Swali: Baada ya kumzika maiti kuna Hadiyth ya kwamba mtu abaki karibu na kaburi la yule maiti kwa kiasi cha muda wa kumchinja ngamia. Hilo lina maana gani?

Jibu: Haya aliusia ´Amr bin al-´Aasw (Radhiya Allaahu ´anh). Alisema:

“Baada ya kuzikwa simameni karibu na kaburi langu kwa kiasi cha muda wa kumchinja ngamia na kuigawa nyama yake.”[1]

Lakini Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwaamrisha Ummah wafanye hivo. Wala hayakufanywa na Maswahabah kutokana na ninavyojua. Pindi Mtume alipokuwa akimaliza kumzika maiti anasimama pembezoni naye na kusema:

“Muombeeni msamaha ndugu yenu na mumtakie uthabiti. Hakika hivi sasa ataulizwa.”[2]

Simama karibu na kaburi lake useme:

“Ee Allaah mthibitishe! Ee Allaah mthibitishe! Ee Allaah mthibitishe! Ee Allaah msamehe! Ee Allaah msamehe! Ee Allaah msamehe!”

Baada ya hapo wanaenda. Kubaki pale ni jambo halikuwekwa katika Shari´ah.

[1] Muslim (121).

[2] Abu Daawuud (3221).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/218)
  • Imechapishwa: 26/08/2021