Inatakiwa kuwa na msimamo wa kati na kati kwa makaburi

Swali: Tunaona namna baadhi ya watu wanavoyapuuza makaburi na wanatembea na kukaa juu yake. Wengine wanayapindukia makaburi na wanayajengea, wanaandika juu yake na wanayawekea mataa. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Waislamu waliozikwa wana haki zao. Makaburi yao yanatakiwa kutembelewa na kusalimiwa na kuombewa rehema na msamaha. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kutembea juu ya makaburi au kukaa juu yake na kusema:

“Mmoja wenu kukaa juu ya kaa likaunguza nguo zake na likaingia mpaka kwenye ngozi yake ni bora kwake kuliko kukaa juu ya kaburi.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza vilevile kuyajengea makaburi na kuandika juu yake na amemlaani yule mwenye kuyawashia mataa.

Ni wajibu kwetu kutozembea kwa ile heshima ya wajibu ya makaburi. Haijuzu kuyatweza, kukaa juu yake na mfano wa hayo. Haijuzu pia kuyapindukia na kuvuka mipaka.

Ni wajibu kwa mtu katika mambo yote kushikamana na Shari´ah na kutahadhari na fitina ya makaburi na kuwa na msimamo wa kupindukia kwayo.

[1] Muslim (971).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/207-208)
  • Imechapishwa: 26/08/2021