Mama amezikwa na mwanamke aliyezikwa miaka mitatu iliyopita

Swali: Mama yangu alikufa alipokuwa na miaka. Akazikwa pamoja na mwanamke mwingine aliyekufa miaka tatu iliyopita. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Haijuzu kumzika pamoja na maiti mwingine maadamu kuna mabaki ya yule maiti mwingine. Kujengea juu ya hili ni wajibu kumzika kila mmoja kwenye kaburi lake. Pindi wanapochimba wakikuta kuna mtu maiti ndani ya ardhi, ni wajibu kurudisha udongo huo na kutafuta kaburi mpya hata kama itakuwa mbali. Muislamu ana heshima yake hata kama ni maiti. Imepokelewa katika Hadiyth:

“Kuvunja mfupa wa maiti ni kama kuvunja mfupa wa aliye hai.”[1]

[1] Ahmad (6/48), Abu Daawuud (3207) na Ibn Maajah (1616).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/215)
  • Imechapishwa: 26/08/2021