Ni lazima kurudisha udongo wote uliochimbwa kutoka ndani ya kaburi?

Swali: Baadhi ya watu wanasema ule udongo uliochimbwa kutoka kwenye kaburi ni lazima kuurudisha wote ndani ya kaburi kwa kuwa ni haki ya yule maiti. Ni sahihi?

Jibu: Si sahihi. Ikiwa udongo unazidi kiasi cha shibri basi haitakiwi kumfukia nao. Makaburi yaliyoinuka zaidi ya shibri ni kwenda kinyume na Sunnah. Wanachuoni wanasema kusizidishwe udongo mwingine juu ya ule udongo uliotolewa ndani ya kaburi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/194)
  • Imechapishwa: 26/08/2021