Swali: Kunatafutwa baraka kwa mabaki yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) tu?

Jibu: Ni mabaki yake yeye tu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kusitumiwe kipimo juu yake kwa wengine. Walikuwa wakitafuta baraka kwa jasho lake, mate yake na yale yaliyoshikana na mwili wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa ajili hiyo ndio maana Maswahabah hawakufanya hivo kwa Abu Bakr as-Swiddiyq, ´Umar, ´Uthmaan, ´Aliy wala mwengine katika Maswhabah wakuu. Kufanya hivo kwa wengine kunaweza kupelekea katika shirki na upetukaji mipaka, tofauti na yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anawabainisha na kuwawekea wazi yale yanayowapasa. Allaah amemfanya kuwa maalum kwa baraka (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24273/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%AA%D8%A8%D8%B1%D9%83-%D8%A8%D8%A7%D8%AB%D8%A7%D8%B1-%D8%A7%D9%84%D9%86%D8%A8%D9%8A-%EF%B7%BA
  • Imechapishwa: 21/09/2024