Ni lazima kusawazisha na kuziba mianya ya safu katika swalah ya jeneza?

Swali: Imeshurutishwa kukamilisha safu ya kwanza baada ya nyingine na kuziba mianya baina ya safu katika swalah ya jeneza?

Jibu: Safu katika swalah ya jeneza zinatakiwa kuwekwa sawa kama swalah zingine na zikamilishwe safu za kwanza baada ya zingine na yazibwe mianya baina ya safu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/110)
  • Imechapishwa: 07/09/2021