Inafaa kwa wanawake kuswali pamoja na wanaume swalah ya jeneza?

Swali: Katika msikiti wa Makkah kunatangazwa kumswalia maiti. Je, inajuzu kwa wanawake kuswali swalah hii pamoja na wanaume sawa ikiwa ni kwa maiti aliyeko pale au ambaye hayupo?

Jibu: Mwanamke ni kama mwanaume. Kukiletwa jeneza aliswalie na anapata ujira kama anaopata mwanaume. Dalili kuhusu hilo ni zenye kuenea na hazikuvua kitu. Wanahistoria wamesema kuwa waislamu walimswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo walianza wanaume kisha wanawake[1].

Kujengea juu ya hili hakuna ubaya. Bali ni katika mambo yanayotakikana pindi kutapoletwa jeneza. Ni sawa kwa wanawake kuswali pamoja na wanaume juu ya maiti huyu40.

[1] Tazama “Siyrat-un-Nabawiyyah” ya Ibn Hishaam (02/230) na Ibn Maajah (1627).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/113-114)
  • Imechapishwa: 07/09/2021