Imesuniwa kufanya safu tatu ikiwa idadi ya wenye kuswali ni ndogo?

Swali: Imesuniwa kufanya safu tatu ikiwa idadi ya wenye kuswali ni ndogo?

Jibu: Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba amesema:

“Hakuna mtu yeyote muislamu anayekufa na akaswaliwa na wanaume ishirini wasiomshirikisha Allaah na chochote isipokuwa Allaah atamsamehe kwao.”[1]

Kadhalika imesihi kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba amesema:

“Hakuna muislamu anayekufa akaswaliwa na safu tatu za waislamu isipokuwa atasamehewa.”[2]

Kuna wanachuoni waliosema kuwa imependekezwa kuwafanya wakawa safu tatu hata kama katika kila moja kutakuwa watu wawili wawili.

Wengine wamesema makusudio ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa hilo ni wingi na wakatumia dalili ya Hadiyth ya pili inayosema:

“… wanaume arubaini… “

Hili ndilo lililo karibu [zaidi na usawa].

Kujengea juu ya hili naonelea kuwa bora zaidi ikamilizwe safu ya kwanza baada ya nyingine. Kukipatikana wingi lengo litakuwa limefikiwa.

[1] Muslim (59) na (948)

[2] Ahmad (04/79), Abuu Daawuud (3166) na at-Tirmidhiy (1028).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/107-108)
  • Imechapishwa: 07/09/2021