Maiti wakiwa wengi waswaliwe pamoja au kila mmoja aswaliwe kivyake?

Swali: Siku ya ijumaa kunakuwa maiti wengi na wanakosa nafasi. Je, waswaliwe swalah moja ndefu au waswaliwe mara nyingi [kila mmoja kivyake]?

Jibu: Wote waswaliwe swalah moja ya kawaida na si ndefu. Imamu arudi nyuma na waswalaji nao warudi nyuma. Haijalishi kitu hata kama safu zitasogeleana. Kwa kuwa hawahitajii kurukuu wala kusujudu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/104)
  • Imechapishwa: 07/09/2021