Inafaa kuwabainishia waswalaji jinsia ya maiti kabla ya swalah ya jeneza?

Swali: Ni ipi hukumu ya kubainisha jinsia ya maiti kama ni mwanaume au mwanamke wakati wa kutaka kumswalia?

Jibu: Ni sawa kukhabarisha juu ya maiti kama ni mwanaume au mwanamke pindi anapowekwa mbele ili kutaka kumswalia ikiwa waswalaji hawajui hilo. Lengo ni ili aombewe du´aa ya kiume, ikiwa ni mwanaume, na du´aa ya kike, ikiwa ni mwanamke. Asipobainisha hilo ni sawa vilevile. Waswalaji ambao hawajui lolote kuhusu maiti huyu wanuie mtu huyu aliyeko mbele yao na swalah inatosheleza. Ni mamoja ikiwa wataomba kwa lafdhi ya kiume:

“Allaahumma Ighfir lahu”

Au kwa lafdhi ya kike:

“Allaahu Ighfir lahaa.”

Huku wakilikusudia jeneza hili liliyoko mbele yao.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/103)
  • Imechapishwa: 07/09/2021