Maiti wakiwa wengi wanapangwa na kuswaliwa vipi?

Swali: Pindi kuna maiti wengi waume kwa wake tunawapanga vipi? Je, tumtangulize karibu na imamu yule ambaye ni mjuzi zaidi au wote ni sawa?

Jibu: Jeneza zinapokuwa nyingi wote wanatakiwa kuswaliwa swalah moja. Atangulizwe [karibu na imamu] mwanaume kwanza kisha mwanamke ambapo mtoto wa kiume anatakiwa kutangulizwa [karibu na imamu] kabla ya mwanamke.

Ikiwa mwanaume ameshabaleghe, mvulana hajabaleghe, mwanamke ameshabaleghe na msichana hajabaleghe wanatakiwa kupangwa namna hii: kwanza atangulizwe mwanaume ambaye kishabaleghe, mvulana ambaye hajabaleghe, kisha mwanamke ambaye kishabaleghe halafu msichana ambaye hajabaleghe na usawa wa kiuno cha mwanamke kiwe usawa na kichwa cha mwanaume.

Ikiwa kumekusanywa maiti wa jinsia moja, kwa mfano kuna wanaume wengi, basi tutamtanguliza karibu na imamu ambaye ni mjuzi zaidi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wale mashahidi ambao walizikwa kwenye kaburi moja, alikuwa akiamrisha atangulizwe kwenye mwanandani [upande wa Qiblah] ambaye amehifadhi sehemu kubwa ya Qur-aan[1]. Hii ni dalili inayofahamisha kuwa yule mjuzi zaidi ndiye ambaye anatangulizwa kumfuata imamu.

[1] al-Bukhaariy (1347).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/102-103)
  • Imechapishwa: 07/09/2021