Ni wapi imamu anaposimama pindi anapomswalia maiti mwanaume na mwanamke?

Swali: Imamu anatakiwa kusimama vipi anapomswalia mwanaume, mwanamke na mtoto?

Jibu: Imamu anatakiwa kusimama usawa na kichwa cha mwanaume na usawa na kiuno cha mwanamke. Haya ni mamoja wakawa wakubwa au wadogo. Mtoto wa kiume mdogo imamu anatakiwa kusimama usawa na kichwa chake na mtoto wa kike mdogo imamu anatakiwa kusimama usawa na kiuno chake kama anavyofanya kwa mwanamke.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/102)
  • Imechapishwa: 07/09/2021