Imesunuliwa kumfungisha maiti mikono kama anayetaka kuswali?

Swali: Baadhi ya wenye kuosha maiti wanapotaka kumvisha sanda maiti wanaweka mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto kama ambaye anaswali. Je, kitendo hichi kimewekwa katika Shari´ah?

Jibu: Kitendo hichi hakikuwekwa katika Shari´ah. Mikono ya maiti inawekwa pembeni.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/97)
  • Imechapishwa: 06/09/2021