Ni kweli kuna tofauti katika masuala haya

Ni kweli kwamba kuna tofauti katika masuala haya, lakini ni kitu gani kinachowaua watu hawa? Watu hawa hawatafiti. Kwa sababu wanachotaka ni kuyaacha mambo kama yalivo na kusema:

”Kuna maoni tofauti katika masuala haya. Kila mmoja achukue kila anachokitaka.”

Hapana! Zipo Hadiyth juu ya masuala haya.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliomba kupewa maji na akapewa. Baada ya hapo kukabaki maji ndani ya glasi. Ni upande gani wa kulia unatakiwa kuzingatiwa hivi sasa?  Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kuliani mwake alikuweko Ibn ´Abbaas. Kushotoni mwake alikuweko Abu Bakr. Akamuuliza Ibn ´Abbaas kama anamruhusu ampe Abu Bakr, lakini Ibn ´Abbaas akakataa ampe mabaki yake mtu mwengine. Hivyo akampa yeye na akasema:

”Fuatisheni kuliani.”

Wewe, ambaye ni mhudumu, umeingia kupitia kule. Upande wako wa kulia ni kule, na si kule.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (548)
  • Imechapishwa: 18/12/2020