Swali: Ni jambo limewekwa katika Shari´ah kwa muadhini kutoa adhaana na huku anapotembea nyumbani ili awakumbushe juu ya swalah?

Jibu: Asitoe adhaana isipokuwa awe amesimama. Haifai akaadhini na huku anatembea. Baadhi ya watu wanasema ´swalini`, jambo ambalo halitakikani. Kwa sababu adhaana inatosha. Lakini akiwaona watu wameketi chini, basi awaamrishe kuswali kwa lengo la kuamrisha mema na kukataza maovu. Vilevile inafaa kwake kugonga milango ya watu kwa ajili ya kuwazindua. Lakini kutembea barabarani na kusema:

“Swalini, swalini… “

ni adhaana ya aina nyingine na ni Bid´ah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (18)
  • Imechapishwa: 18/12/2020