Ni kwanini sipati unyenyekevu na kulia?

Swali: Mimi ni kijana najitahidi kulia wakati ninaposoma Qur-aan, ninaposwali au ninapokumbuka hali za waislamu lakini nashindwa. Ni zipi sababu za hilo?

Jibu: Kuna sababu nyingi. Kutokulia kuna sababu nyingi ikiwa ni pamoja na:

1 – Ususuwavu wa moyo kwa sababu ya maasi na madhambi. Mioyo inapokuwa migumu kunapungua kutokwa machozi. Anapoifanyia hesabu nafsi yake, akamcha Allaah, akaacha maasi na akanyooka juu ya amri yake moyo wake huingiwa na uchaji na macho yakatokwa na machozi.

2 – Kughafilika na minong´ono inayowasilishwa na moyo wake hapa na pale mpaka kunamshughulisha na kunyenyekea na kutokwa na machozi. Anaweza kuwa moyoni mwake ni mchaji lakini wasiwasi ukamzidi mpaka kukamshughulisha na utajo wa Allaah, kumtukuza na kunyenyekea mbele Yake. Anaweza vilevile kushughulishwa na fikira mbalimbali zinazompitikia ambazo zikawa zinamshughulisha.

Kwa hivyo anatakiwa kuukusanya moyo wake katika swalah yake, kisomo chake na wakati wa kumtaja kwake Allaah. Hivo ndivo moyo wake utapata uchaji na kutokwa na machozi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4280/ما-اسباب-عدم-الخشوع-والبكاء-وما-العلاج
  • Imechapishwa: 15/06/2022