Swali: Ni ipi hukumu ya swalah ya mtu mjinga ambaye anasema kile kinachomjia kichwani mwake kwa mfano “Ee Karimu, ee Mwenye kurehemu, ee Mola” wakati ambapo imamu yuko anasoma au anatamka katika hali ambazo hakuna Dhikr ndani yake kama katika hali ya kuinuka kutoka katika kikao cha mapumziko kwenda katika Rak´ah ya pili ambapo husema:

اللهم لك الحمد يا رحمان

“Ee Allaah! Himdi zote njema ni Zako, ee Mwenye kurehemu.”

Jibu: Wanayafanya mambo ambayo hayakuwekwa katika SHari´ah. Lakini swalah zao haziharibiki. Hawatamki maneno ya kawaida. Bali wanaomba du´aa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sa-altu Abiy, uk. 149
  • Imechapishwa: 03/07/2022