Swali: Ni kipi kinachomlazimu mtu ambaye amemwingilia mke wake kwenye tupu ya nyuma? Je, kuna mwanachuoni yeyote aliyehalalisha kitendo hicho?
Jibu: Kumwingilia mke kwa nyuma ni kitendo cha haramu kwa mujibu wa Qur-aan, Sunnah na maimamu wote wa waislamu katika Maswahabah, Taabi´uun na wengineo. Allaah amesema katika Kitabu Chake:
نِسَاؤُكُمْ حَرْثٌ لَّكُمْ فَأْتُوا حَرْثَكُمْ أَنَّىٰ شِئْتُمْ ۖ وَقَدِّمُوا لِأَنفُسِكُمْ
”Wake zenu ni konde zenu. Hivyo basi ziendeeni konde zenu vyovyote mpendavyo na tangulizeni kwa ajili ya nafsi zenu.” (02:223)
Imethibiti katika “as-Swahiyh” ya kwamba mayahudi walisema kwamba mtu akimwingilia mke wake kwenye tupu ya mbele kwa kufanya staili kwa nyuma ya basi atazaliwa hali ya kuwa ni mwenye makengeza. Waislamu wakamuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu jambo hilo ndipo Allaah akateremsha Aayah isemayo:
نِسَاؤُكُمْ حَرْثٌ لَّكُمْ فَأْتُوا حَرْثَكُمْ أَنَّىٰ شِئْتُمْ ۖ وَقَدِّمُوا لِأَنفُسِكُمْ
”Wake zenu ni konde zenu. Hivyo basi ziendeeni konde zenu vyovyote mpendavyo na tangulizeni kwa ajili ya nafsi zenu.”
Shamba ni ile sehemu ya maoteo. Mtoto huzaliwa kwenye tupu ya mbele na sio kwenye tupu ya nyuma.
- Muhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (32/267)
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
Jimaa ya kwenye matiti
Swali: Usiku mmoja nilipokuwa nastarehe na mke wangu shaytwaan alinishawishi na nikamjamii kwenye matiti yake mpaka nikamwaga, kitendo ambacho kinanifanya sina raha. Naomba unijibu hilo na ni ipi kafara ya hilo? Jibu: Kinachotakikana ni mtu kutumia kila kitu kama ipasavyo. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema: نِسَاؤُكُمْ حَرْثٌ لَكُمْ فَأْتُوا حَرْثَكُمْ…
In "Jimaa"
08. Uharamu wa kumwingilia mwanamke kwenye tupu ya nyuma
6- Uharamu wa kumwingilia mwanamke katika tupu ya nyuma Ni haramu kwake kumwingilia katika tupu ya nyuma kwa ufahamu wa Aayah iliotangulia: نِسَاؤُكُمْ حَرْثٌ لَّكُمْ فَأْتُوا حَرْثَكُمْ أَنَّىٰ شِئْتُمْ “Wake zenu ni konde kwenu. Hivyo ziendeeni konde zenu vyovyote mpendavyo.”[1] Dalili ya hilo pia ni zile Hadiyth zilizotangulia. Kuna Hadiyth…
In "Aadaab-uz-Zifaaf"
07. Kutumia staili mbalimbali wakati wa jimaa
5- Namna ya kumwingilia Inajuzu kwake mume kufanya naye jimaa kupitia tupu yake ya mbele kwa kutumia staili yoyote anayotaka; ni mamoja atamwingilia kinyumenyume au kimbelembele [maadamu nia ni kwenye tupu ya mbele]. Amesema (Ta´ala): نِسَاؤُكُمْ حَرْثٌ لَّكُمْ فَأْتُوا حَرْثَكُمْ أَنَّىٰ شِئْتُمْ “Wake zenu ni konde kwenu. Hivyo ziendeeni konde…
In "Aadaab-uz-Zifaaf"