Jimaa ya kwenye matiti


Swali: Usiku mmoja nilipokuwa nastarehe na mke wangu shaytwaan alinishawishi na nikamjamii kwenye matiti yake mpaka nikamwaga, kitendo ambacho kinanifanya sina raha. Naomba unijibu hilo na ni ipi kafara ya hilo?

Jibu: Kinachotakikana ni mtu kutumia kila kitu kama ipasavyo. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

نِسَاؤُكُمْ حَرْثٌ لَكُمْ فَأْتُوا حَرْثَكُمْ أَنَّى شِئْتُم

“Wake zenu ni konde kwenu. Basi ziendeeni konde zenu vyovyote mpendavyo.” (02:223)

Kondo ni ile sehemu ya maoto ikiwa na maana ya tupu. Kwani hapo ndipo hutoa kizazi. Hapa ndipo mtu anatakiwa kumwingilia mke wake. Lakini endapo atamwingilia sehemu nyingine isiyokuwa hapo – mbali na nyuma – udhahiri wa ueneaji wa maneno Yake (Ta´ala):

وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ * إِلَّا عَلَى أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ

“Ambao wanahifadhi tupu zao. Isipokuwa kwa wake zao au wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume, basi hao si wenye kulaumiwa.” (70:29-30)

yanapelekea kujuzu na kwamba inajuzu kwake kustarehe na mke wake vovyote anavyotaka isipokuwa tu kwa nyuma. Haijuzu kwa mwanaume kumwingilia mke wake huko.

Swali: Kwa hiyo ina maana kwamba hakuna dhambi juu yake?

Jibu: Huu ndio udhahiri wa mambo. Dalili ya hilo ni maneno Yake (Ta´ala):

إِلَّا عَلَى أَزْوَاجِهِمْ

“Isipokuwa kwa wake zao.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (01) http://binothaimeen.net/content/6629
  • Imechapishwa: 07/02/2019